April 12, 2014



zenjkijiwe.blogspo.com
 Omar Surur Khalfan, Mwanasheria kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar.
Utowaji hukumu ndogo kwa kesi za jinai ikiwemo makosa ya ubakaji imechangia makosa hayo kuripotiwa kila wakati Zanzibar.
Mwanasheria kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar (DPP), Omar Surur Khalfan, amesema sheria za mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2004 imeanisha adhabu ya kifungo cha miaka 25 hadi 30 ila imetoa mwanya wa kupunguzwa adhabu hiyo.
Akiwasilisha mada katika mafunzo maalumu ya jinsia kwa wanahabari wa vyombo mbalimbali amezitolea mfano mahakama  za mikoa ambazo zinalazimika kutoa adhabu isiyozidi miaka saba ambayo inaokwamisha  kutolewa hukumu sahihi kwa kesi kwa  hata za ukatili wa kimwili.
hata hivyo Surur amefahamisha kuwa mahakama hizo kwa mujibu wa sheria za mahakama zinahitajika kuomba idhini ya mahakama kuu ili hukumu  ya mrefu zaidi ya uliowekwa.
"Makosa haya ya jinai ni mengi sana hivyo hakimu wa mikoa wanalazimika kufanya utaratibu huo ili kutoa hukumu ya kifungo cha zaidi ya miaka 20 hadi 30 ila wengi hawafanyi hivyo ili kuwa fundisho kwa wengine " amesema .
zenjkijiwe.blogspot.comAkizungumzia uchelewaji wa kufunguliwa mashatka kwa kesi za udhalilishaji kwa kusubiri uchunguzi wa vinasaba DNA amesema ushihidi huo si lazima kama itakuwepo taarifa ya dakrtari na taarifa maelezo hasa kwa mtoto chini ya miaka 14 aliefanyiwa vitendo hivyo vya ubakaji.
“Kwahiyo vikwazo hivyo vya kisheria, usuluhishi nje ya mahakama, adhabu ya faini huku kukiwa na mazingira yote ya kumtia hatiani mtuhumiwa inazidisha matukio ya ubakaji na hata kuongeza ndoa za umri mdogo zanzibar”… aliwaarifu wanahabari hao .
Ameshauri kufanyika marekebisho ya haraka kwa baadhi ya sheria zilizopitwa na wakati ili kuziba mianya kwa baadhi ya watendaji wa vyombo vya sheria na kutoa hukumu haraka katika kutoa haki kwa waathirika wa matukio hayo kwa wakatii uliopo.
Amezitaja sheria hizo ni ushahidi, ya ndoa, sheria ya vizazi na vifo na sheria ya watoto iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2011.
Nao washiriki wa mafunzo hiyo walipendekeza kwa Serikali kupitia vyombo vyake vya sheria kuzuia dhamana kwa watuhumiwa wa matendo ya ubakaji yanaoripotiwa katika vuombo vya sheria.
"Kunyimwa dhamana pekee ni adhabu lakini kama mtuhumiwa anapewa anaweza kufanya tena kwa kuhisi kuwa hakuna adhabu itakakayomkabili", amesema Issa Yusuf wa Daily news.
zenjkijiwe.blogspot.com
Baadhi ya washiriki wakiskiliza kwa makini
Husna Mohamed wa gazeti la Zanzibar leo kwa upande wake amedai kuwa sheria ya elimu na ndoa lazima zifanyiwe marekebisho hayo kwani inatoa mwanya wa kutoa haki kwa wanafunzi waliopewa ujauzito au kuolewa kupata haki zao.

 

0 comments:

Post a Comment