Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe Mohammed Baloo na Msimamizi Mkuu wa Jumuiya ya ACRA nchini Tanzania Nicola Morganti wakitia saini ya Makubaliano ya Mradi wa Uhifadhi wa Urithi wa Zanzibar na Kutengeneza Ajira (Zanzibar Built Heritage for Job Creation) mjini Zanzibar
|
Jumla
ya watu elfu kumi na tano mia tisa najuhimko ishirini na mbili watafaidika na Mradi wa
uhifadhi wa urithi wa Zanzibar na kutengeneza ajira utakaogharimu euro
milioni 1,200,000 sawa na zaidi ya shilingi bilioni moja za tanzania.
Mradi
huo wa miaka mitatu unatekelezwa na Jumuiya ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe
(JUHIMKO) kwa kushirkikiana na jumuiya ya ACCRA (Cooperanzione in Afrika e
America Latin).
Akizungumza
katika hafla ya utiaji saini mjini Zanzibar Mwenyekiti wa JUHIMKO Muhammed
Bhaloo amesema mradi huo unalenga kuutunza na kuutangaza urithi wa kiutamaduni
uliopo Zanzibar ili kuchangia ukuaji wa uchumi.
“Walengwa wakuu wa mradi huo ni pamoja na mafundi ujenzi, wajasiriamali,
wamiliki wa majengo ya umma na binafsi, watembeza watalii, walimu 200 na
wanafunzi 10,000 wa skuli za msingi na sekondari pamoja na wananchi wa
kawaida”.amefahamisha Bhaloo.
Ameeleza kuwa kutatolewa na
mafunzo ya muda mfupi ya ujenzi na usimamizi wa uhifadhi wa mjengo ya
kihistoria, kuanzishwa maabara katika chuo kikiu cha taifa suza na
kuandaliwa mtaala ya kufundisha matengenezo ya majengo ya kale na mengine
utakaotumia katika chuo cha karume.
Amesema
JUHIMKO itakuwa msimamizi mkuu wa shuhuli za kutoa taaluma na uelewa kwa
walengwa juu ya historia na urithi wa kitamaduni wa mji mkongwe wa Zanzibar ni
miongoni mwa miji ya urithi wa kitaifa inayotambuliwa na UNESCO.
Msimamzi
wa mkuu wa jumuiya ACRA Nicola
Morganti ameshukuru uongozi wa JUMHIKO kwa hatakati zao za kuhifadhi
historia na utamaduni wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment