Katibu wa taasisi hiyo Khamis Mohamed
Juma amesema hatua hiyo ni kumuezi msaani
huyo alizaliwa katika kijiji hicho mwaka 1880. na kuendeleza historia
za wasanii wengine ili kutoa elimu kwa jamii.
Amehamaisha kuwa taasi hiyo imeamua kukusanya na kuzihifadhi kumbu kumbu za Siti binti Sadi kutokana na mchango mkubwa alioutoa ikiwemo kutetea haki za binaadamu Zanzibar.
Amehamaisha kuwa taasi hiyo imeamua kukusanya na kuzihifadhi kumbu kumbu za Siti binti Sadi kutokana na mchango mkubwa alioutoa ikiwemo kutetea haki za binaadamu Zanzibar.
Ameeleza
hayo katika ziara ya kamati hiyo iliyotembelea katika kijiji hicho cha Fumba wilaya Magharibi Unguja.
Mmoja
wa ndugu wa familia wa marehemu Muharam Mohamed akielelzea historia ya siti bint sadi amesema alikuwa ni
mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wengine wa kizazi kipya kwani alitumia fani ya uimbaji katika kukuza
maadili ya Zanzibar.
Siti
binti Sadi alikuwa ni msanii wa kwanza mkubwa wa kurikodi Taarab aliifanya
Taarab kuwa maarufu kutokana na nyimbo zake za mapenzi zilizobeba ujumbe kwa
kijamii na uchambuzi wa kisiasa na zimesaidia kukuza lugha ya kiswahili
katikanchi mbali mbali za Afrika ya Mashariki
0 comments:
Post a Comment