Bodi
ya Chakula Dawa na Vipozi Zanzibar, imekamata tani 10.1 za mafuta aina ya
Sunflower yenye thamani ya shilingi milioni 39 ambayo hayafai kwa matumizi kwa
binaadamu.
Mafuta
hayo yanayomilikiwa na Said Omar Abdalla yamekamatwa katika maeneo ya Amani
ambako mafuta hayo yamehifadhiwa na kuyafunga upya kwa kuyatoa kwenye chupa za lita moja na kuyaweka katika madumu ya lita tano na lita
ishirini.
Mkuu
wa Kitengo cha usalama wa Chakula wa Bodi hiyo Aisha Suleiman amesema mafuta
hayo ambayo yanamalizika muda wa matumizi mwezi ujao yanaweza kusababisha
athari kwa watumiaji kutokana na kuwa mafuta hayo yamewekwa katika hali
isiyoridhisha.
Amesema
mazingira yaliokutwa mafuta hayo ni kuyabadilisha kutoka katika chupa ya lita
moja na kuyaingiza katika dumu la lita ishirini na lita tano kwa kificho cha
kutojuulikana muda halisi wa mwisho wa matumizi kwa mafuta hayo.
Alifahamisha
kuwa madumu yanayotumika kubadilisha mafuta hayo ya lita 20 yanatumika kutoka
kampuni ya Premium Enterprise ambayo yanaonesha muda wake wa kumalizika 2018
jambo ambalo linalenga hali ya udanganyifu kwa watumiaji.
Aidha
alisema hali ya mafuta hayo haikubaliki kwa matumizi sambamba na ghala hilo
kutosajiliwa na mafuta kutosajiliwa kisheria ambayo hayatambuliki katika bodi
hiyo.
Kwa
upande wa wamiliki wa kampuni ya premier enterprise ambao madumu yao yametumika
kutiliwa mafuta amesema walipata taarifa kwa wasamaria wema kwamba madumu yao
yanatumika kujaziwa mafuta na kuuzwa katika sehemu mbalimbali na waliweza kufuatilia na kutoa taarifa kwa vyombo vya
kisheria.
Wameviomba
vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali dhidi ya wadanganyifu hao ambao
wanaharibu biashara za watu wengine kwa maslahi yao sambamba na kuharibu afya
za watumiaji.
Aliekamatwa
akifanya hujma ya mafuta hayo Said Omar amethibitisha kuwa mafuta hayo hayana
muda mrefu kumaliza muda wa matumuzi na amekiri kuwauzia wauza chipsi ndio
wateja wake wakubwa.
Shehena ya maboksi ya mafuta ya kula yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria |
Mkuu wa Idara ya Usalama na Ubora wa Chakula wa
(ZFDB) Bi. Aisha Suleiman
akizungumza na wandishi wa habari kuhusu
kukamatwa mafuta yaliyoingizwa
nchini
kinyume na sheria yenye thamani ya miliono
|
0 comments:
Post a Comment