Chama
cha Mapinduzi kimempitisha Zubeir Ali Maulid kugombea nafasi ya Spika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar katika
kipindi cha mwaka 2015-2020.
Amepata
nafasi hiyo baada ya kupata kura 55 dhidi ya Pandu Ameir Kificho Spika
aliyemaliza muda wake kukitumikia chombo hicho kwa zaidi ya miaka 20 alipata
kura 11 kura 2 huku zimeharibika katika uchaguzi uliofanyika afisi kuu ya CCM
Kisiwandui.
Akizungumza
na waandishi wa habari Maulid amesema anakabiliwa na changamoto kubwa za kuleta
mabadiliko katika utekelezaji wa chombo hicho ambacho ni moja ya muhimuli wa
dola.
Amesema
atatumia uzoefu alioupata katika kufanya kazi katika taasisi za kutunga sheria
kwa ajili ya kuhakikisha baraza la wawakilishi linafanya kazi inayotakiwa ya
kuisimamia serikali kwa mujibu wa katiba.
Nae
pandu ameir Kificho amesema amekubali kushindwa kwani ni hiyo ni demokrasia na yupo tayari akitakiwa kutoa ushirikiano kwa
vile ana uzoefu mkubwa katika nafasi hiyo wa zaidi ya miaka 20.
Baadhi
ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wamesema mabadiliko hayo ni ujumbe tosha kwa rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuwa wawakilishi wanataka mabadilio makubwa katika
serikali kwa ajili ya kuwatumiki wananchi.
Wagombea
hao waliopitishwa kupigiwa kura na kikao cha Kamati maalum ya CCM kilichofanyika Alkhamis ya Machi 24, 2016 ni miongoni mwa wanaccm tisa waliombwa nafasi
hiyo akiwemo Mahmoud Muhammed Mussa, Mohamed Ali Ahmed, Sadifa Juma, David Mwakanjuki, Perera Ame
Silima na Abdalla Waziri.
0 comments:
Post a Comment