Zanzibar bado inakabiliwa
na tatizo la saratani huku kukisekana mipango bora ya kukabiliana na ugonjwa
huo.
Mwenyekiti wa jumuiya ya
watu wanaoishi na saratani Zanzibar MSAFIRI MARIJANI amezitaja changamoto hizo
ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa Magonjwa hayo katika vituo vya afya,
ukosefu wa vifaa na dawa za tiba na uelewa ni mdogo wa jamii juu ya kujikinga
na saratani.
Akizungumza na waandishi
wa habari ikiwa ni maadhimisho ya siku ya ugonjwa huo duniani amesema Zanzibar haina takwimu kamili ya wagonjwa wa kisukari lakini kiasi ya watu 1000 kutoka
visiwani huo wanapokelewa kila mwaka katika hospitali ya ocean road kwa
matibabu.
Amefhamisha kuwa saratani
ya matiti na shingo ya kizazi ndizo zinaongoza kwa
wanawake Zanzibar na saratani ya tenzi dume inaongoza kwa upande wa
wanaume.
Dkt Marijani ambae pia ni
daktari dhamana wa Magonjwa hayo Zanzibar amefahamisha kuwa tiba za
ugonjwa huo ni ghali sana ila njia pekee ni jamii kubadilisha mfumo wa
maisha ikiwemo kupunguza kula vyakula vya mafuta, kufanya mazoezi, kuache
pombe na uvutaji wa sigara unaochangia asilimia 40 ya aina za saratani.
“Saratani inaweza
kuzuilika iwapo itawahiwa mapema, tuongezeni nguvu kukabiliana nayo
vyenginevyo inaweza kuathiri wananchi wengi kwani gharama ya matibabu yake ni
kubwa na wagonjwa wengi hushindwa na kupoteza maisha,” amesisitiza
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Amewakumbusha wananchi
kuwa saratani ni uvimbe mpya kwenye mwili na baada ya muda mfupi
huzalisha chembechembe zinazosababisha athari kubwa na kama haikuwahiwa
mapema inasababisha donda kubwa na kuwa halitibiki tena.
Nae mkurugenzi wa
utumishi Wizara ya Afya Zanzibar Omar Mwinyi Kondo amesema mapambano ya ugonjwa
saratani unahitaji mikakati endelevu huku akiomba jumuiya hiyo kutochoka
kuelimisha jamii juu ya ugonjwa huo
Akitoa ufafanuzi kuhusu
mkakati wa kukabiliana na matumuzi ya tumbaku Zanzibar ambayo ni miongoni mwa
chanzo kikuu cha ugonjwa huo Mratibu wa kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Zuhura Saleh Ame amesema mkakati
wa kuanzisha sheria ya matumuzi na usimamizi wa tumbaku unaendelea kutokana na matumuzi
yake kuongezwka kwa kadi Zanzibar
Kauli mbiu ya siku ya
Saratani inayoashimishwa kila ifikapo April 4 ya kila mwaka ni MIMI NA WEWE
TUNAWEZA KUJIKINGA NA SARATANI.
Mkurugenzi wa Utumishi na uendeshaji Wizaraya ya Afya Zanzibar Omar Mwinyi Kondo akizungumza na waandishi katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani yaliyofanyika Ofisi ya Jumuiya Mpendae. |
0 comments:
Post a Comment