Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu
wa Tanzania Jaji mstaafu Mark Boman amemuomba aliyekuwa mgombe uraisi kwa
tiketi ya chama cha wananchi CUF Maalimu Seif Sharifu Hamadi
kukubali uamuzi wa kurudiwa kwa uchaguzi mkuu Zanzibar.
Amesema ni vyema akubali maamuzi hayo kwani
kama alishinda atashinda tena kwa vile waliompigia kura katika uchaguzi ulifoutwa
ni wale wale watakao mpigia tena na wanaweza kuongezeka.
Boman ameyasema hayo jijini dar es salaam wakati
akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa maalim kujitangazia kuwa
ameshinda ni suala lilokuwa halikufuata utaratibu hivyo nivyema uchaguzi
ufanyike ili kupata rais wa serikali ya zanzibar.
Aidha amesema ili
kumaliza mgogoro huo kurudiwa uchaguzi ni suluisho pekee lakini ni muhimu
kuwepo masharti ya haki, uwazi pamoja na wagombe na vyama vyao waahidi kukubali
matokeo ya uchaguzi
utakaorudiwa .
Mwenyekiti wa Tume ya
uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha ilifuta matokeo ya uchaguzi huo
uliofanyika visiwani humo kutokana na madai ya kasoro mbalimbali
zilizojitokeza.
Akizungumzia kuhusu
mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ya Tanzania Jaji mstaau Bomani amesema
mchakato huo unatakiwa kuendelea mara moja ili kukamilisha kazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment