December 19, 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shien amesisitiza umuhimu wa tasisi za elimu kuangalia umuhimu wa kutoa elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi ili kulinda maliasili zilokuwepo.
Amesema hayo katika mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) huko Tunguu nje kidogo ya mji wa Zanzibar  ambapo pia aliwatunuku vyeti wahitimu  wahitimu 699 katika fani 15 wakiwemo 7 wa Shahada ya Uzamili ya Sayasi katika Kemia..
Amekitaka chuo hicho kuendelea kufanya tafiti kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo na kuhakikisha kuwa matokeo yake  yanasambazwa kwa taasisi na sekta zinazohusika ili kutumika ipasavyo katika mipango ya maendeleo.
Dk. Shein  
Katika maelezo yake Dk. Shein amesema ameridhishwa na dhamira na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na SUZA za kuimarisha shughuli za utafiti na ubunifu kama alivyokuwa akihimiza na hadi akaanzisha Idara za utafiti kwa kila Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“Matunda ya jitihada zenu tayari yanaonekana tukijua kwamba wakati vyuo vyengine vinakosa waombaji wa kujiunga na masomo, SUZA imepata zaidi idadi inayohitajika tena wakiwa na sifa nzuri zaidi ya viwango vilivyowekwa”,amesema Dk. Shein.
Amewataka wahitimu kuendelea kuwa waadilifu na wazalendo kwa nchi yao na kuwahimiza walioomba mikopo Serikalini kufanya juhudi za kurejesha mikopo hiyo kwa mujibu wa sheria na makubaliano yaliopo ili fedha hizo ziwasaidia wanafunzi wengine wanaotaka kujiendeleza. 
Nae Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idrisa Ahmada Rai, amemueleza Dk. Shein mikakati iliyowekwa na chuo hicho sambamba na mafanikio yaliopatikana  ikiwa ni pamoja na kuanzisha televisheni ya chuo hicho (SUZA TV) itakayotumika kutoa taaluma ya masomo ya sayansi kwa skuli za Sekondari za Zanzibar sambamba na kuitumia TEHAMA kwa kufundishia.




0 comments:

Post a Comment