April 29, 2014

 Kamati ya mifugo, utalii na uwezeshaji ya baraza la wawakilishi imeahidi kufuatilia kwa ka karibu maendeleo ya ujenzi wa soko la samaki la Malindi Zanzibar ili kumalizika kwa wakati uliopangwa.
Ujenzi huo unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu na kumalizika April 2016 kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kwa dola za kimarekani million 9 na Serikali ya Zanzibar itachangia shilingi Million 391.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mlinde Mbarouk Juma amesema ameridhishwa na matayarisho ya ujenzi wa diko na soko hilo la samaki.
Akitoa taarifa kwa kamati hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe ameeleza kamati hiyo kuwa ujenzi huo utakapokamilika wavuvi na wafanyabiashara wakatukwa na  mazingira mazuri  katika soko hilo linalotegemewa na wanachi wengi wa  mji wa Unguja.

0 comments:

Post a Comment