Sekta
ya habari Zanzibar inaendelewa kukabiliwa na changamoto ya sheria zinazowanyima
uhuru wa kupata habari.
Mkufunzi
wa mafunzo ya wandishi wa habari Jasad Bungala ameeleza kuwa katiba ya sasa
haionyeshi kulinda uhuru wa vyombo vya habari tofauti na nchi nyengine duniani.
Amesema
vyongo vingi vya habari vinazuliwa au kunyimwa kupata habari na serikali katika
baadhi ya taasisi zake.
Hivyo
ametoa rai ya kuondoshwa vikwazo hivyo vya kwani inakosesha fursa za mabadiliko
na kukwamisha haki ya kidemokrasi ya kupata habari kwa wananchi iliyowekwa
katika katiba.
Naye
Mkurugenzi wa Kituo cha huduma za sheria Zanzibar kilichoandaa mafunzo hayo
Harusi Miraji Mpatani amesema wananchi wengi wanavunjiana haki zao za
kibinaadamu bila kufahamu na baadae kuitupia lawama serikali kuwavunja haki
Amezitaja
miongoni mwa haki zinazovunjwa ni jamii kuchukua sheria mikononi badala ya
kutoa taarifa kwa wasimamizi wa sheria.
Mkurugenzi
Harusi amewasisitza waandishi hao kutumia nafasi yao kuwaelimisha jamii
kufahamu haki zao na mbinu za kufikia maendelo yao.
0 comments:
Post a Comment