Mtu mmoja amefariki na zaidi ya nyumba mia tisa zimethirika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kisiwa cha unguja usiku wa
kumkia jana.
Waziri wa nchi afisi ya Makamu wa Rais Aboud Mohamed
Aboud amesema mtu huyo Salim Mohamed Kindi mkaazi wa Migombani ngazi mia
amefariki kwa kuangikiwa na ukuta wa nyumba yake.
Akitoa taarifa kuhusu athari za mvua hizo
katika mkoa wa mjini magharibi amesema kutokana na kasi ya maji ya mvua nyumba
nyengine zimebomoka, zimenguka hali iliyowafanya baadhi ya watu kuyahama
makaazi yao huku na miundo mbinu kadhaa ya barabara imeharibika.
Waziri aboud amesema serikali inaendelea
kuchukuwa juhudi za kuwasiaida walioathirika na mvua hizo na inatarajia
kufungua kambi za wahanga mafuriko ya mvua hizo katika maeneo mbali mbali ya
mji.
Akizungumzia hatau za za baadae za kubaliana na mafuriko
yanayotokea kila ifikapo msimu wa mvua amesema serikali inakusudia kubomoa
nyumba zote zilizojengwa katika njia za maji na mabondeni na katika hatau za
awali kiasi nyumba mia tatu zitabomolewa na wakazi watapewa maaeneo ili kujenga
nyumba.
0 comments:
Post a Comment