JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya
kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya
kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia
kufanyika tarehe 20 Machi, 2016
Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la
kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa
majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu. Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote
aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa hizo
zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.
JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia
Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu,
kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es
Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.
0 comments:
Post a Comment