PRESS RELEASE
Zanzibar
28.11.2015
Dk. Shein aliyasema hayo leo, huko katika kwianda
cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja, mara baada ya kufanya ziara ya
kukitembelea kiwanda hicho na kuangalia ukarabati mkubwa wa majengo pamoja na
mitambo yake unaoendelea kufanywa na wawekezaji wa Kampuni ya Shanta Sugar
Holding Lmtd kutoka nchini India.
Katika maelezo yake Dk. Shein aliueleza uongozi wa
Kampuni hiyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi kubwa
zilizochukuliwa na wawekezaji hao zikiwemo za kuanza awamu mpya ya kiwanda
hicho kwa kutumia compyuta na digital katika uzalishaji wa sukari na bidhaa
nyengine zinazotokana na miwa.
Dk. Shein alisisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wa kiwanda hicho kwani mkakati
maalum umewekwa na Serikali kwa kukiimarisha kiwanda hicho kwa kutambua kuwa
hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuimrika bila ya waekezaji.
“Wawekezaji ni lazima wasaidiwe ili waweze kuekeza vizuri”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kusisitiza haja ya kuimarisha uhusiano mwema
kati ya wawekezaji na Serikali ili na wao wapate faida na biashara izidi kuwa
nzuri huku akieleza matumaini yake kuwa wananchi watapata nafuu kubwa ya bidhaa
hiyo mara uzalishaji utakapoanza kiwandani hapo.
Dk. Shein aliwapongeza wawekezaji hao kwa kuekeza
Dola milioni 30 kwa hatua za mwanzo sambamba na juhudi zinazoendelea
kuchukuliwa na uongozi wa kiwanda hicho za kuongeza Dola nyengine milioni 11.5
za Kimarekani katika kukiimarisha kiwanda hicho ambacho kitakuwa na mitambo ya
kisasa na uzalishaji bora wa sukari na bidhaa nyegine zitokazo na miwa.
Dk. Shein alisema kuwa juhudi za wawekezaji hao zimemtia moyo mkubwa ikiwa ni
pamoja na azma yao ya kutoa ajira kwa vijana zipatazo 200 katika sehemu za
kiwandani na 500 mashambani na kuendelea zaidi ajira hizo kwa kadri uzalishaji
utakavyoimarika.
Pia, Dk. Shein alifarajika kwa maelezo aliyoyapata
kutoka kwa uongozi wa Kampuni hiyo wa kueleza kuwa watazalisha umeme wao
wenyewe ambao watatumia kiwandani hapo na mwengine kuweza hata kuliuzia Shirika
la Umeme la Zanzibar ZECO ili kuweza kuwasambazia wananchi vijijini.
Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwahakikishia
wawekezaji hao kuwa maombi yao waliyoyatoa kwake yakiwemo kuongezewa heka 3500
za ziada, maghala ya kuhifadhia biadhaa zao pamoja na nyumba za wafanyakazi ambayo
yote hayo kwa mujibu wa maelezo ya Dk. Shein yatafanyiwa kazi kwa taratibu
maalum za serikali.
Dk. Shein aliwapongeza wawekezaji hao kwa kazi
kubwa walizofanya pamoja na hatua kubwa iliyofikiwa katika uimarishaji wa
kiwanda hicho licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza ambazo zinaendelea
kupatiwa ufumbuzi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alitoa rai kwa
wawekezaji hao kuitumia vyema mbolea watakayoitoa kiwandani hapo kwa kuanzisha
kilimo cha mboga mboga sambamba na kuwasaidia wakuma wadogo wadogo ili na wao
waweze kuzalisha mbogamboga na kuweza kusaidia maendeleo ya Zanzibar
Mapema Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Mhe. Omar Yussuf Mzee alieleza kuwa Mradi wa kiwanda hicho ni muhimu sana kwani
utaimarisha uchumi wa Zanzibar hasa ikizingatiwa kuwa unaunganisha sekta ya
Kilimo hapa nchini.
Mzee alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupitia Wizara yake ya Fedha iliona ipo haja kubwa ya kuunga mkono
Mradi huo kwani utasaidia sana uchumi na maendeleo ya Zanzibar kwani ni mradi
wa Kitaifa na utachangia sana taifa.
Akieleza faida nyengine muhimu mbali ya uzalishaji
wa sukari kutoka kiwandani hapo, Waziri Mzee alisema kuwa kiwanda hicho
kitasaidia suala zima la ajira, umeme, mbolea na kueleza kuwa katika uzalishaji
wa kiwanda hicho hakuna kitakachotupwa.
Nae Mwenyekiti wa Kampuni hiyo ya uwekezaji Bwana
Mahesh Patel alimueleza Dk. Shein hatua mbali mbali zilizofikiwa na kiwanda
hicho katika ukarabati wake mkubwa unaoendelea huku akimuahidi kuwa kiwanda
hicho kitanza kuzalisha sukari mwezi wa
Januari mwakani.
Mwenyekiti
huyo alimueleza Dk. Shein miongoni mwa juhudi za ujenzi na ukarabati
uliofanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi hodhi la kubwa la maji ambalo litasambaza
maji mashambani, azma ya sukari
itakayozalishwa kiwandani hapo kuwa na kuwa na nembo maalum‘Brand’ ya Zanzibar, unafuu wa
bei ya bidhaa hiyo kwa wananchi wa Zanzibar na mambo mengineyo.
Aidha, Mwenyekiti huyo alieleza kuwa hatua hizo
zilizoanza mwaka jana zimefikia pazuri
na kutumia fursa hiyo kueleza kuwa uzalishaji wa kiwanda hicho utasaidia
uchumi wa Zanzibar sambamba na kuweka historia nzuri ya Zanzibar katika
biashara na uwekezaji huku akitoa pongezi kwa Serikali hasa Wizara yake ya
Fedha kwa mashirikiano mazuri wanayoyapata.
Akitoa maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mtendaji
wa Mamlaka ya Maeneo Huru na Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Khamis Nassor, alisema kuwa
ujenzi na ukarabati mkubwa unaoendelea kufanywa na waekezaji hao hasa
ikizingatiwa kuwa zaidi ya mitambo yenye asilimia 80 kiwandani hapo ni chakavu
ambayo itabadilishwa upya una umuhimu mkubwa katika uchumi wa Zanzibar.
Alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa ili haja ya
kiuchumi iweze kutimia hapa Zanzibar na kueleza kuwa muda si mrefu matunda ya
kiwanda hicho yataanza kuonekana
Kambla ya mazungumzo hayo Dk. Shein alitembelea
kiwanda hicho katika maeneo yote na kuangalia hatua za ujenzi zinazoendelea
pamoja na uwekaji wa mitambo mipya, miundombinu ya maji, umeme pamoja na shughuli nyenginezo za kiwanda na
kupata maelezo kutoka kwa viongozi wa kiwanda hicho.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
0 comments:
Post a Comment