April 11, 2014

Kamati Kuu ya Taifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania  inatarajia kuzindua chapisho la tatu la taarifa za msingi za kieneno, kijamii na kiuchumi .


Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua chapisho hilo tarehe 23 mwezi huu katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania .

Mwenyekiti mwenza wa kamati HIYO Balozi Seif Ali Iddi ametoa  taarifa hiyo  katika kikao cha kamati hiyo ya sensa huko Dodoma.
zenjkijiwe.blogspot.com

Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiendesha Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Dodoma.
Akitoa taarifa ya Wizara ya fedha ya Serikali ya tanzania Naibu Waziri mh. Muigulu Nchemba amesema  wizara hiyo inaendelea na maandalizi ya machapisho mengine 10 kuhusu vizazi na ndoa, elimu, uhamiaji na makazi pamoja na hali ya ulemavu kupitia ripoti hiyo ya sensa.
Amezipongeza taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa kwa kusaidia kufanikisha kazi ya sensa hasa katika  upatikanaji wa fedha.

“ …tunawashukuru wadau wetu wa maendeleo  kwa kweli wametusaidia kutuunga mkono katika zoezi hilo kwa zaidi ya shilindi bilioni tatu “. amesema Mh. Nchemba.

Nae Mkurugenzi  Mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Tanzania Dr. Albina Chua akitoa taarifa amesema wamefanya kazi ya uhakiki wa mipaka  ya wilaya za  Tanzania bara na Zanzibar  katika  wilaya za Gairo na Chemba kwa Tanzania bara na Wete na Micheweni kwa upande wa Zanzibar.
zenjwe.b;ogspot.com

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Dr. Alina Chua akitoa Taarifa fupi juu ya uhakiki wa mipaka   ya Wilaya Nchini Tanzania na upande wa kulia ni Bw Mohd Hafidh Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
zenjkijiwe.blogspot.com
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Sensa kutoka Kushoto ni Kamishna wa Sensa Tanzania Bara Hajat Amina Mrisho Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Mh. Muigulu Nchemba na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr. Florens Turuka.
zenjkijiwe.blospot.com
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao ni Wajumbe wa KamatiI Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania wakiendelea na Kikao chao Mjini Dodoma.
 

0 comments:

Post a Comment